1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kompany achaguliwa kuwa kocha ajaye wa Bayern: Rummenigge

29 Mei 2024

Vincent Kompany amechaguliwa kuwa kocha ajaye wa Bayern Munich lakini maelezo kuhusu mkataba wake bado yanapaswa kukamilishwa.

https://p.dw.com/p/4gOcU
Vincent Kompany
Bayern Munich imefikia makubaliano na Vincent Kompany kuchukua mikoba ya Thomas Tuchel aliyefutwa kaziPicha: Tim Markland/PA Images/IMAGO

Mwanachama wa bodi ya klabu hiyo Karl-Heinz Rummenige amesema mkurugenzi wa spoti wa klabu ya Bayern Munich Max Erbel amemchagua Kompany kuwa kocha mpya.

Rummenige, ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 68 ameiambia televisheni ya Sky Italia kuwa kocha wa Manchester City Pep Guardiola aliwasaidia katika chaguo lao. Kompany ana uzoefu wa Bundesliga, baada ya kuichezea Hamburg kabla ya kujiunga na Man City.

Soma pia: Julian Nagelsmann anatakiwa Bayern Munich kumrithi Tuchel 

Alichukua mikoba katika klabu ya Burnley mwaka wa 2022, na kuwapandisha katika Ligi Kuu ya England baada ya kuibuka mabingwa wa daraja la pili msimu huo. Hata hivyo, klabu hiyo ilishuka daraja baada ya msimu mmoja katika Ligi ya Premier. Kompany ndiye mgombea wa karibuni kabisa kwenye orodha ndefu ya makocha waliohusishwa na Bayern.