Kocha wa timu ya taifa ya Tunisia ajiuzulu | Michezo | DW | 29.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kocha wa timu ya taifa ya Tunisia ajiuzulu

Kocha wa timu ya taifa ya kandanda ya Tunisia Georges Leekens amesitisha mkataba wake baada ya kutolipwa mafao yake aliyoahidiwa. Tunisia imesema imeanza harakati za kumtafuta mrithi wake

Georges Leekens

Mbelgiji huyo mwenye umri wa miaka 66 ameiongoza Tunisia kwa mwaka mmoja na aliifikisha timu hiyo katika robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mapema mwaka huu. Aliiongoza nchi hiyo kuichabanga Djibouti mabao nane kwa moja katika mechi za kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika 2017. Taarifa ya shirikisho la kandanda la Tunisia imesema mazungumzo ya kumtafuta kocha mpya wa kigeni yameng'oa nanga.

Leekens amesema kulikuweko na tofauti za maoni kati yake na shirikisho la Tunisia kuhusiana na mafao ya Kombe la Mataifa ya Afrika ambayo hawajalipwa ikiwa ni miezi minne baada ya dimba hilo kukamilika. Mbelgiji huyo alikuwa amesaini kandarasi mpya ya miaka miwili na Tunisia mnamo Machi mwaka jana.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Rueters
Mhariri:Iddi Ssessanga