1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Bundesliga | SC Freiburg vs. Bayer 04 Leverkusen | Christian Streich
Picha: Herbert Rudel/Sportfoto Rudel/IMAGO
MichezoUjerumani

Kocha Streich arefusha mkataba na klabu hiyo ya Freiburg

Bruce Amani
14 Machi 2023

Kocha wa muda mrefu wa klabu ya Freiburg Christian Streich na benchi lake la ukufunzi wamerefusha mikataba yao huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitegemea kuutumia muendelezo mzuri wa mafanikio.

https://p.dw.com/p/4OeVq

Streich amekuwa Freburg tangu 2011 a anashikilia rekodi ya klabu hiyo ya kuongoza mechi 430 katika mashindano yote. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 57 pia sasa ndiye kocha aliyehudumu kwa muda mrefu zaidi katika Bundesliga.

Klabu hiyo haijatoa maelezo ya urefu wa mkataba huo mpya.

Freiburg wamepata mafanikio chini ya Streich kwa kufuzu mara kadhaa katika mashindano ya Ulaya, na habari za kurefushwa mkataba zinajiri siku mbili kabla ya kucheza dhidi ya Juventus katika mechi yao ya mkondo wa pili hatua ya 16 bora.

"Tuna furaha kuwa tutaendelea kufanya kazi na timu yetu ya sasa ya makocha,” alisema mkurugenzi wa Spoti wa Freiburg Jochen Saier katika taarifa.

"Christian Streich na wenzake wanafanya kazi kwa bidi kila siku kwa uwezo wao wote kuhakikisha kuwa timu yetu inaendelea kukua. Tunaendelea kufanya vitu kivyetu na ushirikiano huu wenye mafanikio na wa thamani kubwa utaendelea hadi msimu ujao pia."

Freiburg wanagombania nafasi ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu na kwa sasa wako katika nafasi ya tao katika Bundesliga, pointi saa na RB Leipzig ambao wako katika nafasi ya tatu. Union Berlin inashikilia nafasi ya nne.

Reuters