Wataalamu wanasema kuwa kuna tafauti za maana ya maneno kwenye makamusi kati ya yale yachapishwayo pwani ya Afrika Mashariki na yale yachapishwayo pande za bara. Dk. Mary Zacharia Charwi amefanya utafiti juu ya hilo na hapa anazungumza na Mohammed Khelef.