1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Senegal aombwa kusaidia kutatua mivutano ECOWAS

18 Mei 2024

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amemtolea mwito mwenzake wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, kutumia nafasi yake ndani ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS, kusaidia kutatua mizozo iliyopo huko.

https://p.dw.com/p/4g1ga
Kiongozi wa Senegal aombwa kusaidia kutatua mivutano iliyopo ECOWAS
Rais wa Ghana Nana Akufo-AddoPicha: Kola Sulaimon/AFP

Addo amesema mzozo mkubwa unaotarajiwa kushughulikiwa ni ule baina ya Jumuiya hiyo na mataifa ya Niger, Burkina Faso na Mali.

Mataifa hayo matatu yalitangaza mnamo Januari mwaka huu kujiondoa kwenye Jumuiya hiyo baada ya uanachama wao kusitishwa kufuatia mapinduzi ya kijeshi yalitokea katika mataifa hayo. 

ECOWAS yaangazia namna mpya ya kukabiliana na mizozo ya kikanda

Rais Faye amesema Jumuiya ya ECOWAS, ambayo rais wa Nigeria Ahmed Tinubu ni mwenyekiti wake, inapitia wakati mgumu lakini bado kuna matumaini. Nigeria na Senegal zimeahidi kukuza demokrasia katika eneo la Afrika Magharibi.