1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kiongozi wa Hamas Haniyeh akutana na Ayatollah Ali Khamenei

23 Mei 2024

Viongozi wa muungano unaoongozwa na Iran, "mhimili wa kujihami", akiwemo Ismail Haniyeh wa Hamas, wamefanya mjadala kuhusu vita vya Gaza wakati wa mkutano wao wa mjini Tehran.

https://p.dw.com/p/4gDJR
Iran Ayatollah Ali Khamenei Ismail Haniyeh Mohammad Mokhber
Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei akizungumza na Mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh, Kaimu Rais wa Iran Mohammad Mokhber ameketi kushoto, wakati wa mkutano wao huko Tehran, Iran, Jumatano, Mei 22, 2024.Picha: ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Viongozi wa vuguvugu hili walikutana Jumatano baada ya kuhudhuria shughuli za mazishi zilizoandaliwa mjini Tehran kwa ajili ya heshma za mwisho za Rais Raisi, aliyefariki Jumapili katika ajali ya helikopta kaskazini magharibi mwa Iran. Mkutano huo ulihudhuriwa na Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya Hamas yenye makao yake Qatar, pamoja na naibu wa Hezbollah Naim Qassem na msemaji wa Huthi Mohammed Abdulsalam. Haniyeh pia hapo awali alikuwa na hadhara na kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei.

Ushirikiano wa kimkakati katika eneo la Mashariki ya Kati

Shirika la utangazaji la serikali IRIB limetangaza kuwa mkutano huo pamoja na mambo mengine uliyaweka mezani masuala ya hali ya wakati ya kisiasa, kijamii na kijeshi huko Gaza ikiwemo jukumu la safu ya upinzani. Mkutano huo unaripotiwa kusisitiza kuendelea na mapambano hadi ushindi kamili wa Palestina huko Gaza kwa ushirikiano wa makundi yote katika eneo hilo.

"Mhimili wa kujihami" unawaleta pamoja washirika wa kikanda wa Iran katika mapambano dhidi ya Israel, wakiwemo vuguvugu la Palestina la Hamas, Hezbollah ya Lebanon, Wahuthi wa Yemen na makundi yenye kujihami kwa silaha ya Shia ya Iraq.

Kuuwawa kwa kamanda wa Hezbollah

Lebanon I Israel imeishambulia Lebanon
Watu wakisafisha eneo lililoshambulie na Israeli katika kijiji cha Shehabiya kusini mwa Lebanon mnamo Aprili 16, 202.Picha: Hassan Fneich/AFP

Katika maeneo ya vita Israel imesema imemuua kamanda wa wanamgambo wanaounga mkono Iran Hezbollah kusini mwa Lebanon. Hezbollah ilithibitisha kifo hicho lakini haikutaja cheo cha mtu huyo. Shirika la Habari la Kitaifa la Lebanon (NNA) limeripoti kuwa watoto watatu walijeruhiwa katika shambulio hilo karibu na soko mji wa Nabatiyeh.

Tangu kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza, kumekuwa na makabiliano ya kijeshi ya kila siku kati ya jeshi la Israel na Wanamgambo wa Hezbollah na makundi mengine katika eneo la mpaka kati ya Israel na Lebanon.

Vyanzo viwili vya kiusalama vya Misri vimesema taifa hilo limetoa ahadi ya kuendelea kujitolea kusaidia  kujadili makubaliano ya kusitisha mapigano na kuachiliwa huru kwa mateka hukoGazalicha ya mashaka juu ya jukumu lake la upatanishi, na inawasiliana na Israel kuhusu kupanga tarehe za mazungumzo mapya.

Misri, Qatar na Marekani zimekuwa zikijaribu juhudi za kufanikishwa uwekwaji chini silaha kwa awamu tofauti kati ya Israel na Hamas na kwa awamu kuchiliwa huru kwa mateka wa Israel wanaoshikiliwa katika eneo hilo.

Soma zaidi:Makombora ya anga ya Israel yauwa 35 Gaza

Itakumbukwa tu, Jumatano iliyopita Misri ilionyesha kuwa inaweza kujiondoa katika jukumu la mpatanishi katikati ya mivutano inayohusiana na kukwama kwa mazungumzo ya hapo awali na kusonga mbele kwa jeshi la Israeli katika eneo la kusini Gaza mji wa Rafah

Wizara ya Afya ya Ukanda wa Gaza inayoratibiwa na Hamas inasema zaidi ya Wapalestina 35,800 wameuawa na wengine 80,011 wamejeruhiwa nchini Israel kwa mashambulizi ya Israel tangu Oktoba 7. Lakini pia takribani Wapalestina 91 wameuawa na 21 kujeruhiwa ndani ya masaa 24.

Vyanzo: AFP/RTR