1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Kiongozi wa genge la wahalifu nchini Haiti Ti Greg auawa

22 Machi 2024

Mmoja wa viongozi wa genge la wahalifu nchini Haiti Ti Greg ameuawa katika eneo la Petion-Ville, viungani mwa mji mkuu Port-au-Prince.

https://p.dw.com/p/4e04e
Mwanamke akipita katika moja ya barabara ya Port-au-Prince
Mwanamke akipita katika moja ya barabara ya Port-au-PrincePicha: Odelyn Joseph/AP/dpa/picture alliance

Ernst Julme anayejulikana kama Ti Greg ameuawa katika makabiliano na polisi, siku moja tu baada ya kiongozi mwengine wa genge la wahalifu kuuawa pia katika kile polisi walichoeleza ni kuzuka upya kwa mashambulizi ya makundi hasimu ya magenge.

Ti Greg alikuwa akiongoza kundi la wahalifu la Delmas 95.

Kifo cha Ti Greg ni pigo kwa mipango ya magenge ya wahalifu yalionuia kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya mji mkuu Port-au-Prince. Kiongozi huyo wa genge la wahalifu, hivi majuzi alikuwa ametoroka gerezani.

Soma pia:  Mazungumzo ya kuunda serikali yashika kasi nchini Haiti

Akihutubia mkutano wa waandishi wa habari kutoka Haiti kwa njia ya video, mratibu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wa taifa hilo la kanda ya Karibea Ulrika Richardson amesema shughuli za kila siku nchini humo zimesimama.

Ulrika Richardson ameongeza kuwa idadi kubwa ya watu wameyakimbia makaazi yao baada ya magenge ya wahalifu kuchukua udhibiti wa miji kadhaa.