KINSHASA: Machafuklo yazuka nchini Kongo
27 Oktoba 2006Matangazo
Machafuko yameripotiwa nchini Jamhuri ya Kodemokrasi ya Kongo huku duru ya pili ya uchaguzi wa rais ikiaribia kufanyika mwishoni mwa juma.
Imeripotiwa watu wasiopungua wanne wameuwawa kwenye mapigano kati ya wafuasi wa rais Joseph Kabila na mpinzani wake mkuu Jean Pierre Bemba katika mji wa Gbadolite, kaskazini magharibi mwa Kongo.