KINSHASA : Bemba atishia kuitisha migomo | Habari za Ulimwengu | DW | 25.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA : Bemba atishia kuitisha migomo

Mgombea wa urais alieshindwa nchini Congo Jean Piere Bemba hapo jana amemuonya Rais Joseph Kabila kwamba dhuluma na rushwa zinaweza kuvuruga demokrasia na ametishia kuitisha migomo na maandamano ya upinzani.

Hilo ni shambulio kali la kwanza hadharani dhidi ya rais kutolewa na kiongozi wa zamani wa waasi Bemba tokea akubali kushindwa kwenye uchaguzi mkuu wa kihistoria katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo mwaka jana.

Ametowa kauli yake hiyo kali hadharani ikiwa ni siku chache tu kabla ya ziara ya Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- moon nchini humo na wakati ambapo serikali ya baada ya kipindi cha uchaguzi ikiandaliwa.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com