Kesi ya Zuma yaahirishwa hadi Agosti | Matukio ya Afrika | DW | 17.05.2022
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kesi ya Zuma yaahirishwa hadi Agosti

Kesi ya rushwa inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma imeahirishwa hadi mwezi Agosti.


Mahakama inayoisikiliza kesi hiyo imetangaza mjini Peietermaritzburg kwamba uamuzi huo umechukuliwa kwa sababu mahakama ya juu ya rufaa nchini humo haijatoa hukumu kuhusu rufaa kadhaa za Zuma. 

Mahakama hiyo imeamua kwamba ikiwa uamuzi utapitishwa kuhusu maombi ya mawakili wa Zuma kufikia Agoti mosi, basi kesi yake itaanza tena Agosti 15. Zuma, mwenye umri wa miaka 80, hakuhudhuria kesi yake hivi leo, ambayo ilikuwa imeahirishwa mara kadhaa.

Zuma anashtakiwa kwa rushwa, ubadhirifu wa fedha na ulanguzi kuhusiana na mkataba wa silaha kabla kuwa rais, lakini mwenyewe anakanusha madai hayo. Anakabiliwa na kifungo cha miaka 25 jela iwapo atatiwa hatiani.

Chanzo: afp