1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yawakamata waliojaribu kuingia kambi ya Uingereza

Sylvia Mwehozi
6 Januari 2020

Polisi nchini Kenya wamewakamata watu watatu waliojaribu kuvunja na kuingia katika kambi ya jeshi ya Uingereza mjini Laikipia katika mkoa wa kati wa nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/3VlUe
Karte Kenya Lamu EN
Picha: DW

Polisi nchini Kenya wamewakamata watu watatu waliojaribu kuvunja na kuingia katika kambi ya jeshi ya Uingereza mjini Laikipia katika mkoa wa kati wa nchi hiyo. Haya ni kwa mujibu wa ripoti ya polisi iliyoonekana na shirika la habari la Reuters. Watu hao walikamatwa hapo jana jioni, katika siku hiyo hiyo ambayo Wamarekani watatu waliuwawa na wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al Shabab katika kambi ya kijeshi ya Manda Bay iliyoko karibu na mpaka wa Somalia. Polisi inasema jaribio hilo la kuvunja na kuingia katika kambi hiyo halikufanikiwa na lilinaswa katika kamera za siri. Watu hao waliokamatwa wanahojiwa na maafisa wa kukabiliana na ugaidi.