Kelvin Ruud aanza kazi | Habari za Ulimwengu | DW | 26.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kelvin Ruud aanza kazi

Waziri mkuu mteule wa Australia, Kelvin Ruud, ameshauriana na viongozi mbalimbali duniani kuhusu njia ya kuuidhinisha mkataba wa Kyoto unaotaka gesi zinazotoka viwandani zipunguzwe.

Akianza kazi kufuatia ushindi mkubwa wa chama cha Labour, Kelvin Ruud, atailekeza Australia katika siasa za mrengo wa kushoto, baada ya miaka 12 ya utawala wa kikosavativ.

Ushindi wa chama cha Labour unaiweka Australia katika hali ya kupingana na Marekani kuhusiana na maswala mawili muhimu, Irak na ongezeko la joto duniani.

Ruud amekutana na maafisa wa serikali yake kujadili utaratibu wa kusaini mkataba wa Kyoto, swala alilolipa kipaumbele katika kampeni yake ya uchaguzi.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com