Kipindi cha Karibuni kimemualika msaani wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania Ney wa Mitego. Pamoja na mengine mengi utasikia akizungumzia sakata la kuzuiwa kwa wimbo wake mpya kutokana na sababu za kisheria zilizoelezwa na Baraza la Sanaa nchini Tanzania, BASATA.