Kabul. Watu 12 wauwawa katika ghasia. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul. Watu 12 wauwawa katika ghasia.

Nchini Afghanistan , ghasia zimesababisha watu 12 kuuwawa jana Jumanne. Watu wanne wameuwawa na wengine saba wamejeruhiwa na majeshi ya Marekani katika msako uliolenga dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi kusini mashariki ya Afghanistan. Kwingineko nchini humo, mtu aliyejitoa muhanga ameuwa watu wanane kusini mwa nchi hiyo. Lengo la mtu huyo aliyejitoa muhanga ni gavana wa jimbo la Helmand, Mohamed Daud, ambaye amenusurika , kwa mujibu wa maafisa.

Maelfu kadha ya raia wameuwawa katika mapigano nchini Afghanistan tangu majeshi yanayoongozwa na Marekani kuuangusha utawala wa Taliban mwaka 2001.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com