Juhudi zinazofanywa na shirika la Senegalese Dream
Bruce Amani/Stefan Möhl3 Julai 2015
Fanta Diallo ni muasisi wa shirika la Senegalese Dream – yaani Ndoto ya Senegal, ili kujaribu kuwashawishi vijana wa Kiafrika wanaotarajia kupata kazi Ulaya kuichagua Senegal. Yeye ni mwanaharakati wa kijamii anayeamini kuwa nchi yake ya Senegal ina mustakabali bora.