1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ivory Coast imetangaza kumalizika kwa mzozo wa nishati

4 Agosti 2021

Serikali ya Ivory Coast imetangaza kumalizika kwa mzozo wa nishati nchini humo baada ya wiki kadhaa za mgao wa umeme na matatizo ya kukatika huduma hiyo.

https://p.dw.com/p/3yWx0
Elfenbeinküste,  Yamoussoukro: Stadtansicht
Picha: Getty Images/AFP/S. Kambou

Waziri wa nishati Thomas Camara amesema usambazaji wa umeme umerejeshwa tangu Julai 9 kote nchini humo.

Amewaambiwa waandishi wa habari mjini Abidjan kuwa mpango wa mgawo wa umeme umekamilika baada ya siku 45. Camara ameongeza kuwa ili kuepusha mzozo kama huo katika siku za usoni, taifa hilo la Afrika Magharibi limenunua kiwanda kingine kipya cha hifadhi ya umeme chenye megawati 200 na kukifanyia maboresho kiwanda cha Azito mjini Abidjan.

Katika nyakati za kawaida, uwezo wa Ivory Coast hutosheleza mahitaji ya ndani ya nishati na inayobaki huuzwa katika nchi jirani. Mwaka jana, iliuza asilimia 11 ya nishati yake nchini Ghana, Togo, Benin, Burkina Faso, Mali na Liberia.