1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaharibu kamera 17 za uangalizi za UN nchini Lebanon

4 Aprili 2026

Vikosi vya Israel vimeharibu kamera 17 za uangalizi za makao makuu ya ujumbe wa amani wa Umoja wa Mataifa UNIFIL kusini mwa Lebanon ndani ya saa 24 .

https://p.dw.com/p/5BfJV
Lebanon Tyrus 2026 | shambulizi la Israel
Shambulizi la anga la Israel katika eneo la Al Hosh karibu na mpaka na Lebanon mnamo Aprili 4, 2026.Picha: Kawnat Haju/AFP

Afisa mmoja wa uslama aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina,  amesema kamera hizo ziliharibiwa na jeshi la Israel katika mji wa pwani wa Naqura.

Hapo jana UNIFIL iliripoti kutokea kwa mlipuko katika moja ya kambi zake karibu na Odaisseh kusini mwa Lebanon na kujeruhiwa kwa maafisa wake watatu.

Hata hivyo imesema bado hawajafahamu ulipotokea mlipuko huo.

Kwa upande wake, jeshi la Israel limelishtumu kundi la Hezbollah kwa kurusha roketi iliyoanguka kwenye jengo la UNIFIL .

Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Jakarta imesema leo kuwa waliojeruhiwa ni raia wa Indonesia.

Indonesia imeshtumu tukio hilo na kulitaja kuwa lisilokubalika na kuongeza kuwa matukio hayo yanasisitiza haja ya dharura ya kuimarisha ulinzi kwa vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa.