1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiIsrael

Israel: Uingereza idhibiti chuki dhidi ya Wayahudi

29 Aprili 2026

Wizara ya mambo ya nje ya Israel Jumatano imeitaka serikali ya Uingereza kuchukua hatua za haraka kukabiliana na chuki dhidi ya Wayahudi, kufuatia kisa cha Wayahudi wawili kuchomwa kisu jijini London.

https://p.dw.com/p/5D1NX
Uingereza London 2026 |Operesheni ya polisi baada ya shambulio la kisu huko Golders Green
Uingereza imekumbwa na kisa kingine cha mashambulizi ya Wayahudi, huku ikiongezewa shinikizo la kumaliza visa hivyoPicha: Justin Tallis/AFP

Kupitia mtandao wa X, wizara hiyo imeikosoa serikali ya Uingereza kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo ikiangazia kuanzia mashambulizi kwenye masinagogi, taasisi za Kiyahudi, magari ya wagonjwa ya jamii hiyo hadi kisa hiki cha sasa.

Wizara hiyo imesisitiza kwamba maneno tu hayatoshi kukabiliana na mizizi ya chuki dhidi ya Wayahudi inayoenea kote Uingereza na kuitaka serikali ya Waziri Mkuu Keir Starmer kuchukua hatua na maamuzi ya haraka.

Rais wa Israel Isaac Herzog kwa upande wake amesema ameshtushwa na shambulizi hilo na kusema wakati umefika sasa kwa ulimwengu kuanza kupambana na wimbi hili la kutisha la chuki dhidi ya Wayahudi kwa namna yoyote ile.