1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ISLAMABAD : Wanajeshi 35 wauwawa

8 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCut

Takriban wanajeshi 35 wa Pakistan wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya mshambuliaji wa kujitolea muhannga maisha kujiripuwa kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Msemaji wa jeshi amesema hao waliokufa ni wanafunzi wa kijeshi ambao walikuwako katika kituo cha kujiandikisha na amekiita kitendo hicho kuwa cha kigaidi.

Mripuko huo umetokea katika mji wa Dargai ambao unasemekana kuwa ni ngome kuu ya kundi la wanamgambo linalowaunga mkono watawala wa zamani wa Afghanistan Taliban.