ISLAMABAD : Mashambulizi yauwa watu 51 | Habari za Ulimwengu | DW | 20.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD : Mashambulizi yauwa watu 51

Nchini Pakistan takriban watu 51 wameuwawa katika mashambulizi matatu tafauti ya kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa wakati shinikizo kwa Rais Pervez Musharraf likiongezeka kufuatia msako wa serikali yake dhidi ya Waislamu wa itikadi kali.

Shambulio kwenye msikiti wa jeshi katika mji wa kaskazini magharibi wa Kohat limeuwa watu 15.Mashambulizi mengine mawili ya kujitolea muhanga maisha kwa kujiripuwa moja katika mji wa Hub na jengine kwenye mji wa kaskazini ulioko mbali wa Hangu yameuwa watu 36.

Kwa jumla zaidi ya watu 160 wameuwawa katika wimbi la mashambulizi tokea vikosi vya usalama vya serikali kuvamia msikiti wa itikadi kali mjini Islamabad mapema mwezi huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com