1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Imran Khan afutiwa mashitaka ya mauaji

28 Agosti 2023

Mahakama nchini Pakistan imemfutia mashitaka ya mauaji waziri mkuu wa zamani, Imran Khan, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo chengine kwa hatia ya ufisadi, huku hali ya kisiasa ikizidi kuwa mbaya nchini humo.

https://p.dw.com/p/4VdeC
Pakistans ehemaliger Premierminister Imran Khan
Picha: Mohsin Raza/REUTERS

"Mungu Mkubwa" aliandika wakili wa Khan, Naeem Panjutha, kwenye ukurasa wa X, akiongeza kuwa mahakama imeondoa madai yaliyohusiana na mauaji ya mwanasheria mmoja katika mji wa Quetta kusini mwa nchi hiyo.

Soma zaidi: Kiongozi wa upinzani akamatwa Pakistan kwa kosa la kufichua siri za serikali

Khan aliyefunguliwa madai ya mauaji mwezi Juni, anakabiliwa na kesi zaidi ya 100, tangu alipoondolewa madarakani katika kura ya bunge ya mwezi Aprili ya kutokuwa na imani naye, baada ya mvutano kati yake na jeshi lenye nguvu kubwa la Pakistan.

Mahakama kuu mjini Islamabad pia inatazamiwa kutoa uamuzi wa rufaa iliyowasilishwa na Khan akitaka kusimamishwa madai ya ufisadi dhidi yake hati.