MigogoroUkraine
Vifo na majeruhi wa Urusi na Ukraine huenda wakafika mil.2
29 Januari 2026
Matangazo
Ripoti ya Kituo cha Masomo ya Kimkakati na Kimataifa, CSIS iliyochapishwa siku ya Jumanne imesema watu milioni 1.2 wa Urusi walikufa ama kujeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wanajeshi 325,000 waliokufa katika kipindi cha kati ya Februari 2022 na disemba 2025.
Ripoti hiyo inakadiria kwamba watu 500,000 hadi 600,000 walikufa ama kujeruhiwa nchini Ukraine ambako kuna raia na wanajeshi wachache, miongoni mwao waliokufa ni 140,000.
Takwimu hizo zinachapishwa chini ya mwezi mmoja wa maadhimisho ya miaka minne tangu Urusi ilipoivamia kikamilifu Ukraine Februari, 2024.