1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ibrahim Traore kuapishwa Ijumaa kama rais wa mpito

20 Oktoba 2022

Baraza la kikatiba nchini Burkina Faso limetangaza kuwa Kapteini Ibrahim Traore aliyeongoza mapinduzi ya kijeshi ya hivi karibuni zaidi nchini humo, ataapishwa kuwa rais wa mpito hapo kesho Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4ISGc
Burkina Faso | PK Ibrahim Traore
Picha: AA/picture alliance

Jeshi tayari lilikuwa limetangaza kwamba Traore atachukuwa jukumu hilo la rais wa mpito lakini kuapishwa kwake hapo kesho kutathibitisha hilo rasmi.

Umoja wa Afrika walaani mapinduzi ya hivi punde nchini Burkina Faso.

Baraza hilo la kikatiba limesema jana kuwa linatambua rasmi nafasi ya urais ilioko na kuongeza kuwa katika mkutano wa kitaifa wa vikosi vya kijeshi vya nchi hiyo, Traore mwenye umri wa miaka 34 aliteuliwa kuwa rais wa mpito, mkuu wa nchi na mkuu wa jeshi la kitaifa.

Katika taarifa, baraza hilo limesema, limezingatia kile lilichokiita kujiuzulu kwa Luteni kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba.

Kiongozi wa kijeshi Burkina Faso akubali kujiuzulu

Damiba mwenyewe alinyakua mamlaka mnamo mwezi Januari na kumlazimisha kuondoka madarakani rais wa mwisho wa Burkina kuchaguliwa kwa njia ya demokrasia, Roch Marc Christian Kabore.