Hertha Berlin yailaza Werder Bremen | Michezo | DW | 14.12.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hertha Berlin yailaza Werder Bremen

Hertha Berlin waliwazidi nguvu Werder Bremen kwa kuwachabanga magoli matatu kwa mawili katika mechi iliyochezwa jana ya Ligi kuu ya soka Ujerumani - Bundesliga. Ushindi huo umewasongeza hadi nafasi ya sita

Mshambuliaji wa Hertha Adrian Ramos alitikisa wavu mara mbili katika dakika tisa ili kusawazisha golila kwanza lililofungwa katika dakika ya 15 na Nils Peterson, baada ya kuandaliwa pasi na Aaron Hunt ambaye alicheza mchuano wake wa 200 katika Bundesliga.

Beki wa Bremen Theodore Gebre Selassie alimwangusha Per Skjelbred katika dakika ya 17 kisha Ramos akafunga mkwa mkwaju wa penalti, kabla ya Skjelbred kumwandalia pasi mshambuliaji huyo wa Hertha ambaye alifunga tena. Hunt alisawazisha dakika nne baadaye, kabla ya mpenzi wa mashabiki Ronny kufanya mambo kuwa 3-2 kwa kufunga goli la ushindi.

Champions League FC Bayern München - Manchester City

Bayern waliduwazwa na Manchester City magoli matatu wka mawili katika Champions League

Leo, Jumamosi, viongozi wa Ligi Bayern Munich wanawaalika Hamburg huku Pep Guardiola akitaraji kuwa mabingwa hao wamejifunza kutokana na makosa waliyofanya wakati wa kichapo walichopewa nyumbani na Manchester City.

Bayern wanaweza kuendeleza rekodi yao ya kutoshindwa katika Bundesliga kwa mechi 41 kama watawashinda Hamburg wanaoongozwa na Mholanzi Bert van Marwijk. Hamburg wanamkaribisha nahodha Rafael van der Vaart, lakini mlinda lango Rene Adler yuko mkekani.

Nambari tatu Borussia Dortmund wanacheza ugenini dhidi ya Hoffenheim wakilenga kupunguza pengo la pointi kumi kutoka Kileleni. Borussia wameathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na majeraha kikosini, jambo linalomsumbua kocha Jurgen Klopp. Vijana wa Sammi Hyppia Bayer Leverkusen, ambao wako point inne nyuma ya Bayern, wanachuana kesho Jumapili na Eintracht Frankfurt.

Schalke 04 watawaalika Freiburg, huku kocha wa vijana hao wa samawati Jens Keller, licha ya kufuzu katika awamu ya mtuoano ya Champions League, akiendelea kuwekewa mbinyo huku uamuzi kuhusu hatima yake ukitarajiwa kutolewa wakati wa kipindi cha mapumziko ya msimu wa baridi. Keller atakosa huduma za nahodha Benedikt Hoewedes, ambaye anatumikia adhabu ya kutocheza mchuano huo, pamoja na Julian Draxler ambaye ana jeraha.

Katika menchi nyingine za leo Jumamosi: Hanover 96 v Nuremberg, Mainz 05 v Borussia Moenchengladbach, Augsburg v Eintracht Braunschweig, VfL Wolfsburg v VfB Stuttgart

Mwandishi: Bruce Amani/AFP

Mhariri: Sekione Kitojo