Hecking akasarishwa na uvumi kuhusu de Bruyne | Michezo | DW | 14.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hecking akasarishwa na uvumi kuhusu de Bruyne

Kocha wa Wolfsburg Dieter Hecking anasema amekasirishwa na uvumi wa kila mara katika vyombo vya habari kuhusu ikiwa Kevin de Bruyne atahamia klabu ya Manchester City au la

Miamba wa ligi ya Premier ya England Manchester City wanaripotiwa kujiandaa kumnyakua kiungo huyo nyota Mbelgiji kutoka Wolfsburg.

De Bruyne alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu wa 2014/15 nchini Ujerumani na amekuwa akifanya vyema katika klabu ya Wolfsburg – ambayo ilimaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Bayern Munich katika msimu uliopita – huku akifunga magoli 20 na kuchangia katika magoli 38 katika viwanyang'anyiro vyote tangu alipojiunga nayo kutoka Cheslea mnamo Januari 2014.

Hecking pia anasisitiza kuwa uvumi huo hautakuwa na athari yoyote kwa timu yake wakati ikianzisha kampeni yake ya msimu mpya dhidi ya Frankfurt.

Msimu mpya wa Ligi kuu ya Kandanda Ujerumani umeng'oa nanga rasmi na bila shaka wengi wanabashiri atakayeshinda taji la msimu huu isipokuwa bado ni mapema. Lakini wasimamizi wa mchezo wa kamari hapa Ujerumani wanasema kuwa Bayern Munich ndio wanaopigiw aupatu kushinda taji la kihistoria la nne mfululizo la Bundesliga.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Daniel Gakuba