Hamilton bingwa wa ulimwengu wa F1 | Michezo | DW | 25.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Hamilton bingwa wa ulimwengu wa F1

Lewis Hamilton dereva wa magari ya Mercedes katika mbio za magari za Formula one ameibuka mshindi wa mbio hizo msimu huu , ukiwa ushindi wake wa pili baada ya ubingwa alioupata mwaka 2008.

Hasimu wake katika kinyang'anyiro hicho Nico Rosberg baada ya kupata matatizo katika injini ya gari yake alishindwa kuzuwia ushindi wa mwenzake katika kikosi hicho cha Mercedes. Na Hamilton amehalalisha hatua yake ya kuhamia katika magari ya Mercedes kwa kushinda ubingwa huo na anaamini ni mwanzo tu kwa timu yake na yeye binafsi.

Mercedes itahitaji mazungumzo ya mapema ili kurefusha mkataba na Lewis Hamilton baada ya kupata ubingwa wake huo wa pili mjini Abu Dhabi jana Jumapili.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / ape / rtre
Mhariri: Mohammed Khelef

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com