Hamilton ampiku Rosberg katika mkondo wa Bahrain Grand Prix | Michezo | DW | 07.04.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hamilton ampiku Rosberg katika mkondo wa Bahrain Grand Prix

Na katika mbio za magari ya Formula One, Lewis Hamiltion na Nico Roseberg walipambana vilivyo katika mashindano ya mkondo wa Bahrain Grand Prix, na wakajigamba kuwa wameurejesha msisimko katika mchezo wa F1

Mchezo huo ulikuwa umekabiliwa na malalamiko msimu huu kuwa umeanza kuwa tamasha lisilovutia kutokana na mabadiliko kadhaa ya kiufundi ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya injini za magari ya F1.

Lakini hapo jana, Hamilton alimpiku mwenzake wa timu ya Mercedes Mjerumani Rosberg ili kupata ushindi wake wa kwanza katika mkondo wa Bahrain, ukiwa ni ushindi wake wa 24 katika maisha yake.

Hamilton, ambaye pia alishinda wikendi iliyopita katika mkondo wa Malaysia, alimpiku Rosberg aliyepanda jukwaani katika nafasi ya pili, ikiwa ni ushindi mwingine kwa timu ya Mercedes ambao wameshinda mbio zote tatu msimu huu. Na inaonekana kwamba mwaka huu utawaendea vyema wana Mercedes katika Formula One, lakini acha tuone, kwa sababu msimu bado ni mbichi.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman