Hamilton alishinda mbele ya mashabiki wa nyumbani | Michezo | DW | 06.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Hamilton alishinda mbele ya mashabiki wa nyumbani

Bingwa wa dunia wa mbio za magari za Formula one Muingereza Lewis Hamilton, aliutumia vyema motisha alioupata kutoka kwa mashabiki nyumbani na kushinda mbio za Grand Prix za Silver Stone kwa mwaka wa pili mfululizo

Kutokana na ushindi huo Hamilton sasa nauongoza kwa pointi 17 dhidi ya dereva mwenzake wa timu ya Mercedes Nico Rosberg. Mjerumani Sebastian Vettel alikuwa katika gari aina ya Ferari alimaliza wa tatu, nyuma ya Rosberg.

Mashabiki 140,000 walikuweko kwenye uwanja wa mbio hizo kumshuhudia Hamilton akilinyakua kombe la dhahabu ukiwa ushindi wake wa 38 na wa tano msimu huu.

Hamilton ni muingereza wa tatu kushinda mashindano hayo ya nyumbani ya Silverstone mara tatu, baada ya Jim Clark na Nigel Mansell. Pia kufuatia ushindi huo wa mara ya sita wa nafasi ya kwanza na pili msimu huu, Mercedes imepiga hatua nyengine katika kulitetea taji lake la utengenezaji bora wa magari ikiwa na pointi 371 dhidi ya Ferrari yenye pointi 211.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman
Mhariri: Iddi Ssessanga