1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya Fico inaendelea vyema lakini sio ya kuridhisha

18 Mei 2024

Waziri wa afya wa Slovakia Zuzana Dolinkova amesema hali ya Waziri Mkuu wa taifa hilo Robert Fico inaendelea vyema lakini si yakuridhisha.

https://p.dw.com/p/4g1x3
Zuzana Dolinkova
Waziri wa afya wa Slovakia Zuzana DolinkovaPicha: Vaclav Salek/CTK/picture alliance

Dolinkova ameyasema hayo baada ya Fico kupigwa risasi siku ya Jumatano katika jaribio la kumuua kiongozi huyo wa taifa hilo la Ulaya ya kati. 

Kulingana na Naibu Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Kalinak, hatua ya kumhamisha Fico kutoka hospitali ya mji mdogo alikopigwa risasi wa Handlova, hadi mjini Bratislava haitafanyika ndani ya siku tano zijazo. 

Robert Fico alipigwa risasi mara tano na kujeruhiwa tumboni katika shambulizi lililotajwa kuwa la kisiasa. Madaktari walichukua masaa matano kumfanyia upasuaji wakijaribu kuyaokoa maisha ya mwanasiasa huyo aliye na miaka 59. Madaktari hao wamesema bado Fico ataendelea kuwepo katika chumba cha wagonjwa mahututi. 

Waziri Mkuu wa Slovakia afanyiwa upasuaji mwingine siku mbili baada ya kushambuliwa kwa risasi.

Haya yanajiri wakati mshukiwa aliyeshitakiwa kwa jaribio la kumuua akifikishwa katika mahakama itakayoamua kuhusu kuzuiliwa kwake kabla ya kusikilizwa kwa kesi yake.