Hali katika Kosovo
4 Januari 2009Matangazo
Jumuia ya kujihami ya NATO na Umoja wa Ulaya zimezidisha idadi ya vikosi vyao vya usalama ili kukabiliana na machafuko yaliyoripuka katika eneo la kaskazini la Kosovo.Wazima moto wasiopungua sita wamejeruhiwa katika shambulio la bomu,walipokua wakijaribu kuzima moto katika maduka mawili ya waalbania, yaliyoripuliwa na waserbia katika mji wa Mitrovica.Vikosi ziada vya kulinda amani vya KFOR na maafisa wa polisi wa kikosi cha EULEX wamewekwa mjini humo.Mashambulio hayo yamepamba moto baada ya kuuliwa kiijana wa kiserbia jumanne iliyopita.