1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guterres: Dunia iisaidie Afrika kuwa na nishati jadidifu

5 Septemba 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameutolea mwito ulimwengu kuisaidia Afrika kuwa kanda yenye nguvu kwenye sekta ya nishati isiyochafua mazingira

https://p.dw.com/p/4VySR
Kenia l UN Generalsekretär Antonio Guterres in Nairobi
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Guterres ametoa rai hiyo wakati dunia ikipambana kudhibiti taathira za mabadiliko ya tabianchi. Guterres ameyasema hayo kupitia hotuba aliyoitoa katika mkutano wa bara la Afrika kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaofanyika kwenye mji mkuu wa Kenya, Nairobi. 

Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Afrika inaweza kuistaajabisha dunia kupitia uzalishaji nishati kwa kutumia vyanzo jadidifu na Jumuiya ya Kimataifa inao wajibu wa kutimiza ndoto hiyo.

Mamilioni ya dola kutolewa ili kukabiliana na hewa ukaa

Mkutano huo wa siku tatu mjini Nairobi unawaleta pamoja wakuu wa nchi kadhaa za Afrika, watunga sera na viongozi wa makampuni makubwa kwa lengo la kufikia ajenda ya pamoja kabla ya mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabianchi wa COP28 utakaofanyika huko Umoja wa Falme za Kiarabu.