Guardiola: sijaamua kuhusu mkataba wangu | Michezo | DW | 31.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Guardiola: sijaamua kuhusu mkataba wangu

Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola amekanusha madai kuwa amefanya mazungumzo na vilabu vingine na kuwa timu ya Bayern imeanza kuwa na Kihispania zaidi.

Suala la mkataba wa Guardiola unaokamalika mwaka wa 2016 limezungumzwa katika vyombo vya habari, na Guardiola amejibu madai hayo akisema hajafanya uamuzi kuhusu ikiwa atasaini mkataba mpya.

Mhispania huyo anasema hajapokea maombi yoyote kutoka vilabu vingine ulimwenguni akiongeza kuwa kwa sasa anafurahia kuwa katika klabu ya Bayern na kuwa bado kuna muda wa kuzungumza.

Kuwasili kwa Vidal kutoka Juventus kumeongeza idadi ya wachezaji wanaozungumza Kihispania katika klabu ya Bayern, ambapo Wahispania Javi Martinez, Xabi Alonso, Juan Bernat and Thiago Alcantara tayari wako kwenye kikosi hicho pamoja na Guardiola.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Khelef