1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia zaendelea mjini London

7 Agosti 2011

Wafanyaghasia kaskazini mwa mji wa London wamechoma moto magari ya polisi na wamepora maduka hapo jana, baada ya kuandamana kupinga kuuawa kwa mtu mmoja aliepigwa risasi na polisi siku ya alhamisi.

https://p.dw.com/p/12CPn
Gari la polisi lililochomwaPicha: AP

Zaidi ya watu 200 walikusanyika karibu na kituo cha polisi cha Tottenham kabla ya maandamano hayo kugeuka kuwa vurugu. Polisi mjini London imesema, wafanyavurugu waliwarushia chupa maafisa wa polisi waliokuwa kwenye doria na waliyatia moto magari ya polisi na basi moja.

Siku ya alhamisi, tukio la kufyatuliana risasi na polisi, lilisababisha kifo cha mwanaume mwenye umri wa 29. Polisi wanasema, uchunguzi unafanywa kuhusu kifo hicho.

Mwandishi: Sudi Mnette

Prema Martin