Gbagbo aapishwa kuwa rais | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 05.12.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Gbagbo aapishwa kuwa rais

Rais aliyeko madarakani Laurent Gbagbo ameapishwa rasmi kuwa rais jana Jumamosi nchini Ivory Coast

default

Rais aliyeko madarakani nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo,kulia akipongezwa baada ya kuapishwa.

Rais aliyeko madarakani Laurent Gbagbo ameapishwa rasmi kuwa rais nchini Ivory Coast katika sherehe iliyotangazwa moja kwa moja katika televisheni, licha ya jumuiya ya kimataifa kupinga ushindi wake katika uchaguzi. Wakati huo huo huku hali ya wasi wasi ikiongezeka katika mji mkuu Abidjan , mgombea wa upinzani Allasane Ouattara pia ameapishwa kuwa rais.

Elfenbeinküste / Alassane Ouattara / Wahl

Kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara.

Hapo mapema umoja wa Ulaya na Umoja wa mataifa ulimpongeza Ouattara kwa ushindi wake katika uchaguzi huo. Mjini Brussels, mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema kuwa matokeo ya uchaguzi ni lazima yatambuliwe. Rais wa Marekani Barack Obama amemtaka Gbagbo kukabidhi madaraka. Kumekuwa na taarifa kama hizo kutoka Ufaransa , nchi ambayo ni mtawala wa zamani wa kikoloni wa Ivory Coast.Wamarekani wametakiwa kutotembelea Ivory Coast kutoka na hali ya wasi wasi wa usalama. Gbagbo , ambaye anaungwa mkono na jeshi , alitangazwa mshindi wa uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili wa duru ya pili na baraza la katiba la nchi hiyo, na kubadilisha matokeo ambayo yanaonyesha kuwa Ouattara ameshinda.

 • Tarehe 05.12.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QPxf
 • Tarehe 05.12.2010
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/QPxf
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com