1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 kuisaidia Ukraine kwa kutumia mali za Urusi ilizozizuia

Lilian Mtono
25 Mei 2024

Kundi la Mataifa tajiri ulimwenguni la G7 limesema linajadiliana juu ya namna watakavyotumia mapato ya baadaye ya mali za Urusi walizozizuia ili kuisaidia Ukraine.

https://p.dw.com/p/4gHAr
Mkutano wa Mawaziri wa Fedha wa G7 nchini Italia
Mawaziri wa Fedha wa G7 katika mkutano wao nchini Italia: 24.05.2024Picha: Italy Photo Press/IMAGO

Wakuu wa taasisi za kifedha wa kundi hilo wamesema hayo hii leo, hii ikiwa ni kulingana na rasimu ya taarifa ambayo shirika la habari la Reuters limepata nakala yake.

Kundi la G7 limezuia  mali za Urusi zenye thamani ya dola bilioni 300 , muda mfupi baada ya kuivamia Ukraine, Februari 2022.

Duru kutoka kwenye kundi hilo zimesema rasimu hiyo haitafanyiwa marekebisho makubwa kabla ya toleo la mwisho kutangazwa rasmi baade hii leo.