1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Flick asifu timu yake baada ya kuichakaza Atletico

Deo Kaji Makomba
22 Oktoba 2020

Kocha wa klabu ya Bayern Munich Hansi Flick alisifu ufanisi wa timu yake kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Atletico Madrid ya Uhispania katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa barani Ulaya, siku ya Jumatano

https://p.dw.com/p/3kHBA
UEFA Awards Hansi Flick
Hansi Flick, kocha wa klabu ya Bayern Munich.Picha: Robert Hradil RvS/Reuters

Wahispania hawakuwa sawa kwa washindi wa mataji matano ambao walidhibiti mchezo tangu mwanzo na hawakuwahi kuwaruhusu wapinzani wao kujiangalia wakati walipoanza utetezi wa taji lao kwa kupata ushindi mnono.

"Mchezo wetu ulikuwa mzuri tu usiku wa leo," Flick aliwaambia waandishi wa habari. "Ilikuwa kazi ngumu, lakini tuliijua. Ufanisi wetu ulikuwa mzuri leo na nimeridhika sana. Ni muhimu kushinda mchezo huo wa kwanza."

Bayern walishinda taji la Ligi ya Mabingwa mnamo Agosti, moja ya mataji matano waliyoshinda mwaka 2020, na walikuwa na maandalizi mafupi ya kabla ya msimu, lakini Flick alisema wachezaji wake walipigania kila mpira dhidi ya Atletico.

"Tulikuwepo kimwili. Hiyo ilikuwa muhimu, kuwapo, kushinda hali hizo moja kwa moja. Tulikuwa na mpango wa mechi na tuliutumia, tukifunga mabao manne mazuri. "Tunaweza kuridhika nayo na ndio muhimu. Kwa kweli, tulitaka kushinda mchezo wa kwanza leo," alifafanua Flick.

Bayern, ambao sasa wameshinda michezo yao 12 mfululizo ya Ligi ya Mabingwa, walikuwa makini katika safu ya ushambuliaji na Kingsley Coman alifunga mara mbili na Corentin Tolisso na Leon Goretzka kila mmoja alifunga bao moja.

Bao la kwanza la Coman lilihitaji kugusa mpira kwanza na kudhibiti krosi ya Joshua Kimmich wakati la pili lilikuwa darasa la jinsi ya kumchukua beki kwa hali ya moja kwa moja na kupachika bao la pili.

"Tulicheza vizuri sana usiku wa leo. Nilifunga mabao mawili na ninafurahi sana. Tuna timu nzuri sana na tuna uwezo wa kucheza vizuri pamoja," Coman alisema. "Natumai tunaweza kuendelea."

Chanzo/Reuters