Fernando Alonso arejea katika Malaysia Grand Prix | Michezo | DW | 27.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Fernando Alonso arejea katika Malaysia Grand Prix

Dereva wa magari ya Formula One Ferando Alonso amethibitisha hali inayoizunguka ajali iliyomkumba ya kabla ya kuanza msimu mpya ambayo ilimlazimu kukosa mbio za mwanzo wa msimu za Australia

Mhispania huyo amesema hakuwahi kupoteza fahamu na kuwa hakupatwa na matatizo ya kumbukumbu kutokana na ajali hiyo. Na wakati akijiandaa kwa mashindano ya kesho ya Malaysia, Alonso amesema ""ni furaha kuwa hapa kwa msimu mwingine wa Formula One. Nnaanza hapa kwa kuchelewa, lakini kwa bahati mbaya ajali ya Barcelona, na kufuatia ushauri wa madaktari nilikosa mbio za kwanza lakini nina furaha kuwa hapa...Malaysia kwa kawaida huwa mkondo mzuri kwangu katika taaluma yangu ya Formula One. Nimeshinda hapa mara tatu na timu tatu tofauti. Najua itakuwa kazi ngumu mwaka huu kurudia mafanikio hayo lakini nina furaha kurudi mashindanoni na tayari kufurahia wikendi"

Alonso alihama kutoka timu ya Ferrari na kujiunga na McLaren mwishoni mwa msimu uliopita lakini utata unaozunguka ajali aliyoipata wakati wa majaribio ya magari mjini Barcelona ulizisha maswali mengi kama angeweza kurejea tena katika mashindano ya Formula One.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com