Ferguson akasirishwa na kadi nyekundu | Michezo | DW | 06.03.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ferguson akasirishwa na kadi nyekundu

Meneja wa Manchester United Sir Alex Ferguson alikuwa amekasirika mno na hakuweza kuzungumza na waandishi habari baada ya timu yake kuondolewa katika kinyang'anyiro cha Champions League jana(05.03.2013).

Manchester United's Nani, 2nd left, is shown a red card during the Champions League round of 16 soccer match against Real Madrid at Old Trafford Stadium, Manchester, England, Tuesday, March 5, 2013. (AP Photo/Jon Super)

Kadi iliyozusha hasira za Ferguson dhidi ya Nani

Ushindi wa mabao 2-1 wa Real Madrid ambao ulibadilika baada ya mchezaji wa Man U kuonyeshwa kadi nyekundu ulitosha kuipa mkono wa kwa heri katika mashindano ya mwaka huu.

Ferguson alikasirishwa na uamuzi mkali wa refa wa kumtoa nje mshambuliaji wa pembeni Nani, uamuzi uliosababisha wenyeji hao kubaki na wachezaji 10 uwanjani kwa muda wa dakika 35 za mchezo na kuiruhusu Real kubadilisha matokeo ya mchezo huo kwa mabao ya Luka Modric na Cristiano Ronaldo. Wahispania waliingia katika duru ya robo fainali kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-2.

Manchester United's manager Sir Alex Ferguson speaks at a press conference at Old Trafford Stadium in Manchester, Tuesday, May 3, 2011. Manchester United will play Schalke in a Champion's League semi-final second leg soccer match on Wednesday. (Foto:Jon Super/AP/dapd)

Meneja wa Man U, Alex Ferguson

Pambano jingine siku ya Jumanne la timu 16 bora lilikuwa kati ya Borussia Dortmund na Shakhtar Donetsk, ambapo Borussia ilifanikiwa kuwasambaratisha wageni wao kwa mabao 3-0 na kupata ushindi wa mabao 5-2 , baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa mwanzo nchini Ukraine.

Borussia Dortmund's Felipe Santana (2nd R) and teammates celebrate a goal against Shakhtar Donetsk during the Champions League soccer match in Dortmund March 5, 2013. REUTERS/Ina Fassbender (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER)

Borussia Dortmund waisambaratisha Schachtar Donezk

Ferguson amtuma naibu wake

Mjini Manchester badala ya kuzungumza na waandishi habari , Ferguson ambaye alikuwa amekasirika mno alimtuma msaidizi wake Mike Phelan.

Phelan amesema kuwa kadi nyekundu dhidi ya Nani ilikuwa uamuzi mkali sana , na kwamba hatua aliyoichukua refa huyo kutoka Uturuki Ceneyt Cakir iliharibu mchezo wa jana.

''Tuliamini kuwa tumeudhibiti mchezo kwa mbinu. Tulikuwa katika hali tulivu wakati wa mapumziko ilipokuwa sare ya bila kufungana.'' Alisema Phelan.

Real haikustahili kushinda

Kocha wa Real Jose Mourinho amesema kuwa hana hakika juu ya uamuzi wa refa, lakini Real haikustahili kushinda.

"Tunafurahi kuwa tunasonga mbele, lakini nilitarajia mengi zaidi kutoka kikosi changu, amesema Mourinho. Iwapo mlinda mlango wenu ndio mchezaji bora katika timu, inaonesha kuwa hamuudhibiti mchezo kama inavyostahili. Hatukucheza vizuri."

Mfungaji wa bao la ushindi la Real Cristiano Ronaldo amesema: "Nilicheza hapa kwa muda wa miaka sita kwa hiyo ilikuwa ni siku maalum kwangu kurejea tena hapa na kuonana na marafiki wa zamani. Kama nilivyosema , nafurahi kwamba tumeshinda lakini ni chungu kwa Manchester."

Real hata hivyo ina rekodi mzuri dhidi ya Manchester United. Real imefanikiwa mara nne kuiondoa Man U katika kinyang'anyiro cha Champions League katika michezo mitano waliyocheza.

Mjini Dortmund , Borussia ilipata kazi rahisi dhidi ya Shakhtar Donetsk, kutokana na magoli yaliyowekwa wavuni na Felipe Santana, Mario Goetze na Jakub Kuba Blaszczkowski.

Wajerumani hawakuwa na matatizo makubwa dhidi ya Shakhtar ambayo ilibanwa katika eneo la kiungo na kuwa na matatizo kadha upande wa ulinzi.

Mlinzi kutoka Brazil Santana aliwapa wenyeji Borussia goli la kuongoza katika dakika ya 31 kwa bao la kichwa.

Na kisha Goetze alipachika bao la pili dakika sita baadaye kutokana na pasi kutoka kwa Lewandowski.

Kocha wa Dortmund Juergen Klopp aliueleza mchezo huo kuwa , " ni tukio la kupendeza sana."

Borussia Dortmund's coach Juergen Klopp smiles before the German first division Bundesliga soccer match against Borussia Moenchengladbach in Dortmund September 29, 2012. REUTERS/Ina Fassbender (GERMANY - Tags: SPORT SOCCER HEADSHOT) DFL RULES TO LIMIT THE ONLINE USAGE DURING MATCH TIME TO 15 PICTURES PER GAME. IMAGE SEQUENCES TO SIMULATE VIDEO IS NOT ALLOWED AT ANY TIME. FOR FURTHER QUERIES PLEASE CONTACT DFL DIRECTLY AT + 49 69 650050

Kocha wa Dortmund Jürgen Klopp

"Muda wote wa msimu huu wa Champions League umekwenda vizuri sana kwetu," amesema.

Mario Goetze ameongeza kuwa : "tulifahamu kuwa tuna nafasi kubwa ya kufika robo fainali, na tumecheza vizuri sana."

Kocha wa Shakhtar Mircea aliwamwagia sifa kem kem Dortmund: "Leo ilikuwa kibarua kigumu kweli kweli kuweza kuwashinda....Tulipata nafasi, na inasikitisha kuwa hatukuweza kuzitumia."

epa03208943 Fc Juventus' players jubilate after scoring during Italian Serie A soccer match between Cagliari and Juventus at Nereo Rocco Stadium in Trieste, Italy, 06 May 2012. EPA/MAURIZIO BRAMBATTI

Juventus Turin watataka kumalizia kazi waliyoianza huko Glasgow

Leo Jumatano (06.03.2013) ni duru nyingine ya timu nne kati ya timu 16 zinazopambana kuwania kuingia katika robo fainali, ambapo Juventus Turin ikiwa nyumbani inaikaribisha Celtic Glasgow baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 mjini Glasgow wiki mbili zilizopita na Paris St Germain ikiwakaribisha Valencia baada ya ushindi wao wa mabao 2-1 nchini Hispania.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae / rtre

Mhariri: Gakuba Daniel

DW inapendekeza