F1: Vettel auanza msimu kwa ushindi | Michezo | DW | 27.03.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

F1: Vettel auanza msimu kwa ushindi

Katika tuangalie mbio za magari ya Formula One ambapo msimu mpya umeng'oa nanga rasmi hapo jana nchini Autsralia na ushindi wa kwanza ukamwendea bingwa wa dunia mara nne Sebastian Vettel

Mjerumani Vettel wa timu ya Ferrari alishinda mbio hizo za Australia Grand Prix na kuyawekea doa matumaini ya timu ya Mercedes ya kuendeleza udhibiti wao katika msimu wa nne mfululizo.

Vettel alivurumisha gari lake na kupata ushindi wake wa 43 mbele ya Lewis Hamilton wa Mercedes, huku dereva mwenza wa Muingereza huyo Valtteri Bottas akimaliza wa tatu. Ulikuwa ushindi wa Vettel wa nne katika gari la Ferrari na wake wa kwanza tangu mbio za Singapore Grand Prix mwezi Septemba mwaka wa 2015. Na sasa Mjerumani huyo anasema yuko tayari kupambana msimu huu. "Ni safari ndefu sana. Nadhani kwa sasa tunafurahia tu na kusherehekea. Kimekuwa kipindi kigumu. Zimekuwa mbio nzuri. Mwanzoni sikuwa na furaha sana. Nilikuwa na uwoga. Bila shaka tulikuwa na bahati wakati Lewis alipoondoka barabarani lakini tuliendelea kujikakamua tu. magurudumu yalikuwa sawa na gari lilifanya kazi vizuri".

Dereva mwenza wa Vettel katika mwaka wa 2007 Kimi Raikkonen alimaliza wan ne, huku dereva wa timu ya Red Bull Max Verstappen akifunga nafasi ya tano bora.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Yusuf Saumu