F1: Rosberg ashinda Bahrain Grand Prix | Michezo | DW | 04.04.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

F1: Rosberg ashinda Bahrain Grand Prix

Dereva wa mashidnano ya magari ya Formula Mjerumani Nico Rosberg wa timu ya Mercedes ametwaa ubingwa wa mkondo wa Bahrain Grand Prix. Lewis Hamilton alimaliza wa tatu nyuma ya Kimi Raikonnen wa Ferrai

Baada ya kupata ushindi mara mbili wa mbio za ufunguzi wa msimu, dereva Nico Rosberg amejawa na matumaini makubwa lakini anasema anahofia kitisho cha Ferrari, kufuatia dhihirisho la uwezo wao katika mbio za jana za Bahrain Grand Prix

Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 30 anaongoza orodha ya ubingwa wa madereva duniani akiwa na pointi 17 mbele ya dereva mwenzake wa Mercedes, bingwa mtetezi Lewis Hamilton.

Rosberg anasema anafahamu kuwa Kimi Raikkonen ambaye alimaliza wa pili mbele ya Hamilton aliyepanda jukwaani wa tatu, alidhihirisha kasi ya kutisha katika siku ambayo mwenzake wa Ferrari Sebastian Vettel alishindwa kuanza mbio kutokana na hitilafu ya injini.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com