1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yadai vikosi Tigray vyajiandaa kwa mashambulizi

12 Juni 2026

Mamlaka katika eneo la Tigray nchini Ethiopia imekanusha leo madai kwamba inajiandaa tena kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe na ikaishtumu serikali ya shirikisho kwa kutafuta kisingizio cha kurejea kwenye mzozo.

https://p.dw.com/p/5FIL6
Ethiopia , Tigray , Amanuel Assefa TPLF
Kiongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF, Amanuel AssefaPicha: Million Hailesilassie/DW

Katika mahojiano na shirika la habari la AFP naibu kiongozi wa Chama cha Ukombozi wa Watu wa Tigray TPLF Amanuel Assefa, amesema madai hayo ni "si ya kweli kabisa.

Assefa alidai kuwa serikali inajiandaa kuanzisha vita dhidi ya Tigray  na inataka kutumia kisingizio hicho kuupotosha jumuiya ya kimataifa.

Hapo jana , serikali ya nchi hiyo ilidai kuwa vikosi vya Tigray vilikuwa vinajiandaa kuanzisha mashambulizi dhidi yake katika siku zijazo, jambo lililoibua hofu ya kurejea kwa vita.

Pia iliishtumu  TPLF kwa kuimarisha uhusiano wake na Eritrea, ingawa kundi hilo limekanusha madai hayo.