1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Eritrea yaanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Somalia

Sekione Kitojo
30 Julai 2018

Marais wa Somalia na Eritrea wametia saini makubaliano ya kuanzisha mahusiano ya kibalozi baada ya uhasama wa zaidi ya muongo  mmoja, katika  hatua  ya  kasi  kubwa  ya  kukaribiana hivi  karibuni.

https://p.dw.com/p/32KnG
Bildkombo l Somalischer Präsident Mohamed Abdullahi Mohamed und Eritreische Präsident Isaias Afwerki

Ziara  ya  siku  tatu  ya  rais  wa  Somalia  Mohamed Abdullahi Mohammed  mjini  Asmara  nchini  Eritrea  inaingiliana  na  hatua ambayo  si  ya  kawaida  ya  hatua  za  amani  baina  ya  Eritrea  na Ethiopia , sehemu  ya  mabadiliko  ya  kushangaza   katika  eneo hilo ambalo  lilikabiliwa  na  vita , mizozo inayowahusu  mahasimu ambayo  inachochewa katika  nchi  nyingine , kutengwa  na  utawala wa  mkono  wa  chuma.

Somalia Partnership Forum in Brussels
Rais wa Somalia Mohamed Abdillahi MohamedPicha: picture-alliance/AA/D. Aydemir

"Nchi hizo  mbili  zitaanzisha  mahusioano  ya  kidiplomasia  na kubadilishana  mabalozi," imeeleza  tamko  la  "pamoja  kuhusu uhausiano  wa  kindugu" lililotiwa  saini  mjini  Asmara  na  rais  wa Eritrea  Isaias Afwerki  na  Mohammed  wa  Somalia.

Tamko  hilo  limekuja  kiasi  wiki  tatu  baada  ya  Ethiopia  na Eritrea  kutangaza  mwisho  wa  miongo  miwili ya  mzozo  wao, na kurejesha  mahusiano  ya  kidiplomasia  kwa  haraka  na  safari  ya anga  kati  ya  miji  yao mikuu.

Historia  ya  mataifa  hayo  matatu , na  mtengano  wao , vinakwenda  pamoja.  Somalia  na  Eritrea  zilikuwa  mwanzo  karibu. Chini  ya  dikteta  wa  somalia siad Barre , utawala  wa  kijeshi  mjini Mogadishu  uliunga  mkono  mapambano  ya  muda  mrefu  ya  kudai uhuru  kutoka  Ethiopia, ambao  waliupata  mwaka  1993.

Mwaka  1998  Ethiopia  na  Eritrea  zilianza  kupigana  vita  vya miaka  miwili  kuhusiana  na  suala  la  mpaka  wao  ambavyo vilisababisha  watu 80,000 kupoteza  maisha kabla  ya  kuingia katika  vita  vikali  baridi.

Somalia Anschlag in Mogadischu
Shambulio la kujitoa muhanga karibu na ikulu ya rais wa Somalia mjini MogadishuPicha: Reuters/F. Omar

Vita vya kihasama 

Baada  ya  kuanguka  kwa  utawala  wa  Barre  mwaka  1991, Somalia  ilitumbukia  katika  machafuko na  vurugu.

Ilipofika  mwaka  2006 , Somalia iligeuka kuwa  eneo  kama wachunguzi  wanavyosema  la  vita  baina  ya  Eritrea  na  Ethiopia.

Ethiopia  ikiunga  mkono  serikali  dhaifu  ya  mpito  mjini  Mogadishu wakati  Eritrea  ilishutumiwa  kuunga  mkono  wanamgambo  wa Kiislamu  wanaopigana  kuiangusha  serikali , madai  ambayo inayakana.

Somalia Kismayo
Picha ya angani ya kusini mwa SomaliaPicha: Imago/ZUMA Press/S. Price

Baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  mataifa  mwaka  2009  liliweka vikwazo  vya  silaha  na  vikwazo  vilivyowalenga  baadhi  ya viongozi dhidi  ya  Eritrea kwa  madai  ya  kwamba  inaunga  mkono kundi  la  Kiislamu  lenye  mahusiano na  wanamgambo  wa  al-Shabaab , ambalo liliendelea  kufanya  mashambulizi  yake  ya  mara kwa  mara  licha  ya  kupoteza  maeneo  katika  miaka  ya  hivi karibuni.

Tamko  hilo  rasmi  la  pamoja  limeweka  msisitizo  maalum  katika uungaji  wake  mkono  kwa  serikali  ya  Somalia.

"Eritrea  inaunga  mkono kwa  dhati  uhuru  wa  kisiasa, uhuru  na mipaka  ya  Somalia pamoja  na  juhudi  za  watu  na  serikali  ya Somalia  kurejesha  hadhi  halali  ya  nchi  hiyo  na  kufanikisha matarajio  ya  watu  wake,"  limesema tamko  hilo. Waraka  huo , uliowekwa  katika  tovuti  ya  wizara  ya  habari  ya  Eritrea , pia umesema  mataifa  hayo  mawili, " yatafanya  jitihada  kutengeneza ushirikiano  wa  kisiasa, kiuchumi, kijamii, kitamaduni pamoja  na ulinzi  na  usalama.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe

Mhariri: Yusuf Saumu