Eritrea inatakiwa kuviondoa vikosi vyake Ethiopia | Matukio ya Afrika | DW | 16.04.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Eritrea inatakiwa kuviondoa vikosi vyake Ethiopia

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Linda Thomas-Greenfield ameitaka Eritrea kuondoa wanajeshi wake nchini Ethiopia mara moja.

Matamshi yake yanafuatia kikao cha ndani cha baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na mzozo uliolikumba jimbo la Tigray nchini Ethiopia.

Balozi huyo ameelezea masikitiko juu ya taarifa za ubakaji na matukio mengine yasiyosemeka ya unyanyasaji wa kingoni yanayoendelea kujitokeza kwenye eneo hilo.

soma zaidi: Wanajeshi wa Eritrea waliingia Tigray-akiri Abiy Ahmed

Awali, Mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa Mark Lowcock aliliambia baraza hilo kwamba unyanyasaji wa kingono umekuwa ukitumika kama silaha ya vita katika jimbo hilo la Tigray, hatua iliyomsukuma balozi huyo kuhoji kuhusu umuhimu wa maisha ya watu weusi mbele ya baraza hilo.

Lowcock amesema mzozo wa kibinaadamu umezidi kuchacha katika kipindi cha mwezi uliopita, huku kukiwa na changamoto ya ufikishwaji wa misaada ya kiutu na watu wakifa kwa njaa.