1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW yazindua chaneli ya YouTube ya Kituruki, +90

29 Aprili 2019

Deutsche Welle na washirika wengine watatu wakuu wa kimataifa wa habari wamezindua chaneli mpya ya YouTube inayofahamika kama +90. Wanalenga kuimarisha uhuru wa kujieleza na wa habari nchini Uturuki

https://p.dw.com/p/3Hc1J
Türkei l Youtube-Sperre
Picha: picture-alliance/dpa/K. J. Hildenbrand

Deutsche Welle na washirika wengine watatu wakuu wa kimataifa wa habari wamezindua chaneli mpya ya YouTube ambayo wanasema inalenga kutoa "aina tofauti ya uandishi mpya wa habari" kwa watumiaji nchini Uturuki, pamoja na Waturuki wanaoishi ng'ambo.

DW imeshirikiana na BBC, France 24 na Voice of America kutengeneza chaneli hiyo na itaungana nao katika kutoa maudhui ya video. Mashirika hayo manne ya utangazaji yamesema chaneli hiyo itahusisha mada mbalimbali za maswala ya siasa za kijamii kupitia ripoti, habari za uchambuzi na mahojiano.

PK Start des türkischsprchigen YouTube Kanals +90 (Huseyin Aldemir)
Wawakilishi wa F24, DW, BBC na VOA wakati wa uzinduziPicha: DW/Huseyin Aldemir

Habari za uhakika, maoni huru

"Tunataka kutumia chaneli yetu ya YouTube kuwapa watazamaji taarifa halisi ambazo zitawasaidia kutoa maoni yao wenyewe," alisema Mkurugenzi Mkuu wa DW Peter Limbourg, aliyeongeza kuwa kuwa "huu kwa hakika ni ushirikiano wa kipekee na mashirika ya kimataifa ya habari ukilenga kutoa maudhui kwa wafuatiliaji wanaozungumza Kituruki, ambao wanapenda siasa za kimataifa, biashara, sayansi na utamaduni."

Limbourg na wawakilishi kutoka washirika wengine watatu wa mashirika ya utangazaji wanaizindua chaneli hiyo ya YouTube katika kikao cha leo Jumatatu cha waandishi wa habari mjini Instanbul.

Kufungua dirisha kwa Ulaya

PK Start des türkischsprchigen YouTube Kanals +90 (Huseyin Aldemir)
Mkurugenzi mkuu wa DW Peter LimbourgPicha: DW/Huseyin Aldemir

Mradi huo ni sehemu ya Mpango wa Kimkakati wa DW 2018 -2021, ambao unaeleza kuwa kinyume na matumaini ya wengi, serikali ya Uturuki sasa inaendelea kudhirisha ubabe wake.

Mpango huo unasema DW inalenga kuyadhihirisha maadili ya Ulaya katika masuala ya siasa ya kijamii nchini Uturuki. Malengo ya aina hiyo yanatoa changamoto kubwa kwa soko la Uturuki, kama unavyosema mpango huo: Kazi ya uandishi wa habari nchini Uturuki inaendelea kuwa ngumu; vyombo vyovyote vinavyotaka kuwa washirika wapya vinazidi kukataa ushirikiano na mashirika huru ya habari kutoka nchi za Magharibi." Mpango wa DW ambayo ni shirika la utangazaji la kimataifa la Ujerumani linalofadhiliwa na walipakodi uliidhiniswha na Bunge la Ujerumani Juni mwaka jana.

Pongezi za wanasiasa

Mkurugenzi Mkuu Limbourg aliwasilisha chaneli mpya ya YouTube ya Kituruki bungeni mwanzoni mwa mwezi Aprili. Wawakilishi kutoka vyama vyote bungeni walielezea uungaji mkono wao kwa mradi huo, wakisema kuwa ulistahili kuwepo muda mrefu uliopita. Limbourg alisisitiza ukweli kuwa DW na washirika wake wanazingatia sana maudhui ya uandishi wa habari yasiyoegemea upande wowote.

Mamilioni ya watumiaji duniani kote

Erkan Arikan Kommentarbild App
Erkan Arikan, mkuu wa Idhaa ya DW Kituruki Picha: DW/B. Scheid

DW karibuni ilitanua mahusiano ya ushirikiano wake na kampuni ya France Medias Monde – FFM ambayo inamiliki televisheni ya France24 na mashirika hayo mawili yatachapisha mfululizo wa habari za uchaguzi wa Ulaya kwenye mitandao yao ya kijamii na tovuti zao za intaneti. Lakini chaneli ya YouTube ni ya kipekee, kwa sababu ni ya kwanza kuzileta pamoja televisheni nne za kigeni katika mradi wa pamoja.

DW hutoa habari zilizo huru katika lugha 30. Kwa pamoja, DW na FFM huwafikia watu milioni 320 kila wiki kupitia habari za televisheni, radio na intaneti.

BBC huwafikia watu milioni 279 kila wiki kupitia habari zake za televisheni, redio na intaneti. Mshirika wa nne, VOA, ni shirika kubwa kabisa la utangazaji la kimataifa nchini Marekani. Hutangaza katika zaidi ya lugha 40, na kuwafikia watu milioni 275 kila wiki.