DW moja kwa moja kwenye simu yako kupitia WhatsApp | Masuala ya Jamii | DW | 13.09.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

DW moja kwa moja kwenye simu yako kupitia WhatsApp

Sasa shabiki wa DW popote pale ulipo unaweza kupokea habari, picha, vidio na sauti zenye ujumbe wa kukuchangamsha moja kwa moja kwenye simu yako ya mkononi kupitia huduma ya DW WhatsApp.

Sasa Idhaa ya Kiswahili ya DW inawasiliana nawe moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Sasa Idhaa ya Kiswahili ya DW inawasiliana nawe moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Huduma hii ni mpya na haina malipo yoyote kupitia mtandao wa WhatsApp. Ni rahisi sana kujiunga na huduma hii. Unachohitaji ni simu yako tu yenye huduma ya intaneti na pia WhatsApp. Baada ya hapo, ingia kwenye kiungo cha DW Kiswahili WhatsApp na jaza namba yako na kisha tuma kwa kufuata maelekezo yaliyowekwa hapo.

Baada ya hapo, tutakuweka kwenye orodha ya watu wanaopokea ujumbe kutoka kwetu kila tunapotuma taarifa mpya.

Kuwa mmoja wa marafiki zetu kwenye jamii ya DW WhatsApp, uwe karibu kabisa na habari mpya na ujumbe wa moja kwa moja kwenye simu yako. DW iko nawe popote ulipo.

Mueleze na rafiki yako kwa kumtumia link yetu hiyo. Huduma hii ni ya bure kabisa.

Viungo vya WWW

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com