Dortmund yagonga ukuta kumsajili Witsel | Michezo | DW | 02.08.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dortmund yagonga ukuta kumsajili Witsel

Borussia Dortmund inaelekea  kugonga mwamba katika nia yake ya kumfungisha mkataba mchezaji wa kati wa timu ya taifa ya Ubelgiji  Axel Witsel kutoka klabu ya Tianjin Quanjian ya China katika dirisha la sasa la uhamisho.

EURO 2016 Spielerfrisuren Frisuren Axel Witsel (picture-alliance/dpa/V. Pesnya)

Axel Witsel

Dortmund  inaripotiwa kuwa  tayari  kuzindua  kifungu  cha  ununuzi  cha  euro  milioni  20  katika  mkataba  wa Witsel , lakini   kocha  mkuu  wa  klabu  ya  Quanjian  Paulo Sousa  alionekana  kuzima uhamisho  huo  wa  nyota  huyo  wa  kombe  la  dunia  katika  mktaba  wake  unaoenda   hadi Disemba  2019.

Sijapata  taarifa  zozote kuhusu  uhamisho  wa  Witsel, hata  kutoka  katika  klabu  ama mchezaji  mwenyewe," Sousa  aliliambia  shirika  la  utangazaji  la  CGTN  nchini  China.

"Naelewa  kwamba  mchezaji  huyo  ana  kifungu  cha  uhamisho  katika  mkataba  wake, lakini  kifungu  hicho kinaweza  tu  kufunguliwa  wakati  wa  dirisha  la  uhamisho nchini China. Wakati  huu  ambapo dirisha  la  uhamisho  nchini  China  limefungwa  hapo  julai 12, uhamisho  hauwezi  kufanyika.

"Nina  amani  kwamba  Witsel atarejea. Ni  sehemu  kamili  ya  kikosi  chetu."

Mmiliki  wa  klabu  ya  Quanjian Shu Yuhui amerudia  msimamo  huo  wa  Sou