1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund wamaliza msimu katika nafasi ya pili

21 Juni 2020

Na katika kandanda la Ujerumani - Bundesliga, Werder Bremen inakabiliwa na kitisho cha kutumbukia katika ligi ya daraja la pili baada ya kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Mainz.

https://p.dw.com/p/3e6Mg
Bundesliga I RB Leipzig - Dortmund
Picha: Getty Images/AFP/R. Hartmann

Na katika kandanda la Ujerumani - Bundesliga, Werder Bremen inakabiliwa na kitisho cha kutumbukia katika ligi ya daraja la pili baada ya kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya Mainz. Wenzao katika nafasi ya mkia kwenye msimamo wa ligi Fortuna Duesseldorf, kwa upande mwingine, bado wana nafasi ya kuendelea kupambana katika vita vya kuepuka kushushwa ngazi baada ya kutoka sare ya 1 -1 na Augsburg.

Borussia Dortmund walijihakikishia nafasi ya pili kwenye ligi nyuma ya Bayern Munich baada ya kupata ushndi wa 2 - 0 dhidi ya RB Leipzig ambao wapo katika nafasi ya tatu. Bayern Munich waliwacharaza Freiburg 3 -1. Borussia Moenchengladbach pia waliwapiku Bayer Leverkusen katika vita vya tiketi ya Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa 3 - 1 dhidi ya washika mkia SC Paderborn. Leverkusen walilazwa 2 - 0 na Hertha Berlin.