Dortmund tayari kuumana na Gladbach | Michezo | DW | 07.11.2014
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Dortmund tayari kuumana na Gladbach

Borussia Dortmund wanataka kuitumia hali yao nzuri katika Ligi ya Mabingwa barani Ulaya ili kuyaimarisha matumaini ya ligi ya nyumbani - Bundesliga, watakapowaalika Borussia Moenchengladbach Jumapili

Dortmund walipata ushindi wa nyumbani wa magoli manne kwa moja dhidi ya Galatasaray katika mchuao wa katikati ya wiki ambao ulisitishwa mara mbili kutokana na fataki zilizokuwa zikirushwa uwanjani na mashabiki. Shirikisho la soka Ulaya, UEFA linachunguza tukio hilo.

Ulikuwa ushindi wa nne wa BVB katika jukwaa la Ulaya ambao uliwaweka moja kwa moja katika awamu ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa na kuwaweka juu ya kundi lao. Lakini matokeo yao ya nyumbani ni ya kukera sana baada ya kushindwa mechi tano za mwisho mfululizo katika Bundesliga hali ambayo imewaacha wakijikuna vichwa katika nafasi ya pili kutoka nyuma.

Na sasa Jurgen Klopp ana nafasi nyingine ya kubadilisha mambo dhidi ya Gladbach ambao wako katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi. Glabach mecheza mechi 17 bila kushindwa mchezo wowote na walitoka sare ya kutofungana goli katika mechi ya mwisho dhidi ya BAYERN

Bundesliga 10. Spieltag FC Schalke 04 FC Augsburg

Kocha wa Schalke Roberto Di Matteo anatafuta ushindi wake wa nne katika mechi sita

Pep Guardiola amesema Bayern sasa italenga kuimarisha pengo lao la uongozi la points nne katika Bundesliga, baada ya kupata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Roma katika Champions League, ambao uliwapa tikiti cha kufuzu katika hatua ya mchujo.

Bayern wanashuka dimbani leo dhidi ya Eintracht Frankfurt. Bayern watakosa huduma za beki wa kushoto David Alaba ambaye anauguza jeraha la goti na atakuwa mkekani hadi mwaka ujao.

Bayer Leverkusen watakosa huduma za wachezaji watano wa kikosi cha kwanza, akiwemo nahodha Simon Rolfes katika mchuano wa wa leo dhidi ya Mainz, baada ya ushindi wao wa mbili kwa moja dhidi ya Zenit St Petersburg katika Champions League. Kocha Roger Schmidt atawakosa viungo Gonzalo Castro, Stefan Reinartz na Mgiriki Kyriakos Papadopoulos, wakati beki Tin Jedvaj akitumikia adhabu

Nambari mbili kwenye ligi Wolfsburg wanatafuta ushindi wao wa saba mfululizo watakapowaalika Hamburg kesho Jumapili. Schalke ambao wanashikilia nafasi ya nane, wanalenda kujinyanyua kutokana na kichapo cha Champions League cha magoli manne kwa mawili dhidi ya Sporting LISBON wakati wakiwa ugenini kupambana na Freiburg.

Freiburg wameshinda mechi zao mbili za mwisho na kusonga juu kutoka nafasi ya mkia hadi ya 16 wakati Roberto Di Matteo akitafuta ushindi wake wan ne katika mechi sita tangu aliposhika usukani.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu