1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund, mabingwa wa Kombe la Ujerumani

14 Mei 2021

Borussia Dortmund imeiadhibu RB Leipzig kwa kichapo cha mabao 4-1 na kuibuka mshindi wa kombe la Ujerumani kwa mara ya tano.

https://p.dw.com/p/3tNyR
Fußball: DFB-Pokal Finale I RB Leipzig vs Borussia Dortmund
Picha: Martin Rose/AFP/Getty Images

Kocha wa RB Leipzig Julian Nagelsmann alikuwa na matumaini ya kumaliza muda wake kwa ushindi kabla ya kuhamia Bayern Munich msimu wa joto. Badala yake, timu yake ilivunjwa na kikosi cha Dortmund kilichokua na njaa ya ushindi bila ya huruma. soma Fainali ya Kombe la Ujerumani; Leipzig na Dortmund

Dortmund ilionyesha motisha zaidi tangu dakika ya kwanza ya mchezo, wakiongozwa na Erling Haaland ambaye dhamira yake ya kutamba kimchezo ilijitokeza dhahiri kwa kila hatua ya mchezo. Walimkamata "Red Bull" pembe kuanzia mwanzo wa mechi hadi kipenga cha mwisho.

Makinda wa Dortmund watamba

Deutschland Bundesliga Borussia Dortmund - FC Augsburg | Tor Sancho
Sancho, Reus na Haaland wa DortmundPicha: Sascha Steinbach/AP Photo/picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Makinda wa Dortmund Jardon Sancho na Erling Haaland walifunga mabao 2 kila mmoja. Nahodha wa Dortmund Marco Reus alisaidia katika magoli yote yaliofungwa na kuinyima Leipzig ushindi wao wa kwanza.

``Tukihisi kusukumwa ukutani, basi hapo ndio tunaonyesha thamani yetu, tunapaswa kuendelea kufanya hivi katika miaka mingine ijayo.'' alisema Reus.

Haaland alirudi uwanjani baada ya kuwa nje kwa wiki tatu kutokana na jeraha la msuli. Kunako dakika ya 28 Haaland alimpiku Dayot Upamecano na kuifungia bao la pili Dortmund, na kabla ya kukamilika kwa kipindi cha kwanza Sancho alishirikiana na Reus kupachika wavuni bao la kukamilisha kipindi cha kwanza kwa 3-0 dhidi ya "Red Bulls".

Katika kipindi cha pili Leipzig ilirudi na nia ya kujibu kipigo kwa kufyatua mikaju miliwi iliyogonga mchuma wa lango la Dortmund na kumtia jamba jamba mlinda lango Roman Burki.

Bao la kufuatia machozi, Leipzig 

Deutschland Berlin | DFB Pokal Finale | RB Leipzig v BVB Borussia Dortmund
Picha: Maja Hitij/POOL/AFP/Getty Images

Dani Olmo aliipa Leipzig bao la kufutia machozi kupitia mkwaju maridadi kutoka nje ya eneo la adhabu kunako dakika ya 71 ya mchezo.

Na hatimaye Haaland alifunga mchezo kwa kufunga bao la nne kunako dakika ya 87 na kumuacha kipa wa Leipzig Peter Gulacsi akiduwaa.

Dortmund imewahi kushinda kombe la ujerumani mwaka 1965, 1989, 2012, 2017 na mwaka huu 2021 itakua mara ya tano kulibeba kombe la Ujerumani.

Leipzig, ambayo iliundwa mwaka 2009, ilikuwa na hamu ya kushinda kombe hilo kwa mara ya kwanza lakini ilishindwa kuidhibiti Dortmund.

``Tumefika hapa mara mbili katika kipindi cha miaka miwili na tunambulia kujificha kwa mara ya pili, bila shaka ni uchungu,'' alisema Mkurugenzi mkuu wa Leipzig Oliver Mintzlaff, ambaye timu yake ilipoteza 3-0 dhidi ya Bayern katika fainali ya mwaka 2019.

 

 https://p.dw.com/p/3tK5m