1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund hawakuwa katika likizo licha ya mshituko wa matokeo

Deo Kaji Makomba
18 Juni 2020

Dortmund mashakani kumaliza ligi katika nafasi ya pili

https://p.dw.com/p/3dz9N
UEFA Champions League Finale (FC Bayern München gegen Borussia Dortmund)
Kikosi kazi cha DortmundPicha: Reuters

Nchini Ujerumani klabu ya soka ya Borussia Dortmund watahitaji kucheza kufa na kupona Jumamosi tarehe (20.06.2020) wakati watakapokuwa wakikabiliana uso kwa uso na timu ya RB Leipzing ambayo inatafuta kujihakikishia nafasi ya kucheza ligi ya Mabingwa kwa msimu ujao na kunyakua nafasi ya pili kutoka katika klabu ya bonde la Ruhr.

Dortmund, tayari iko katika zile nafasi nne za juu kuelekea kumalizia msimu wa Bundesliga, wamekwishacheza nusu ya pili nzuri katika msimu lakini mshtuko walioupata kwa matokeo ya kufungwa mabao 2-0 na timu ya FSV Mainz 05 Jumatano tarehe (17.06.2020) yamewaweka Dortmund katika mashaka kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya pili.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Dortmund Michael Zorc, kabla ya mchezo huo wa Jumatano, alionya kwamba wanataka kudhihirisha ukweli kwamba klabu yake ndio namba mbili katika soka la Ujerumani, lakini walionekana kama klabu ya chini katika msimamo kuliko klabu bora zaidi ya pili kwenye ligi ya Bundesliga.

"Tulicheza kana kwamba wengine wetu walikuwa likizo,"alisema Zorc baada ya kushindwa katika mchezo huo na kuiacha Dortmund ikiwa na alama 66 kibindoni ikiizidi Leipzig alama 3.

Kwa upande wake kocha mkuu wa timu ya Dortmund Lucien Favre, alipoulizwa ikiwa wachezaji wake tayari wameamua kumaliza msimu alisema kuwa sivyo na kuongeza kuwa, "tunafahamu kwamba imekuwa msimu mrefu, mwezi na nusu kwa sababu ya hali ilivyo hivi sasa. Unaweza kufikiria ni kama shuleni ambapo unasema kuna wiki moja iliyobaki sio hivyo kwa sisi tunaotoa asilimia 100 kwa kila mchezo."

Vijana wa Caro Ancelott watamani kupindua meza

Wakati hayo yakichomoza nako nchini England ndoto za timu ya everton kuikabidhi timu ya Liverpool taji la ligi kuu na ushindi katika mchezo utakaopigwa Jumapili tarehe (21.06.2020) huko Goodison Park lakini vijana wa Carlo Ancelott, bado watatamani kugeuza meza dhidi ya wapinzani wao.

England Liverpool vs. Sheffield United
Mchezaji wa Liverpool Mohamed Salah kushoto akipongezana na wachezaji wenzake baada ya kufunga goli lake la kwanza wakati wa mechi ya ligi kuu kwenye uwanja wa Anfield Liverpool ilipocheza na Sheffield United, Jan 2, 2020Picha: picture-alliance/AP Photo/J. Super

Ushindi wa mabao 3-0 iliyoupata timu ya Manchester City inayoshikilia nafasi ya pili, dhidi ya Asernal Jumatano iliyopita imeirejesha kwenye hatua baada ya kusimamishwa kufuatia mripuko wa virusi vya corona inamaanisha kwamba Liverpool bado wanahitaji alama sita ili kupata taji la kwanza baada ya kipindi cha miaka 30.

Ushindi huko Goodison na kisha dhidi ya Crystal huko Anfield kungelinda ushindi huo wa kwanza nyumbani wa ligi kuu.

Ingawa ushindi wa Everton katika mchezo wa derby unaweza kuiacha Liverpool ikiwa bado haijakamilisha biashara yake kabla ya kukutana na City mnamo Julai 2.

Kuongoza kwao kwa alama 22, ni nzuri sana na kwamba matokeo ya taji hayaeleweki lakini jambo la mwisho kwa Klopp na timu yake wanataka baada ya miezi mitatu ya kusimamishwa kwa ligi hiyo itakuwa na wiki zaidi kungoja kupata kombe mikononi mwao.

Katika hali ya kawaida Liverpool ingekumbana na umati wa watu wenye uadui uliojaa ndani ya anga kubwa la Goodison lakini kwa sasa mchezo huo utapigwa bila ya mashabiki na kuifanya ile faida ya Everton kuchezea nyumbani kupotea.

Takwimu za kitafiti kutoka kwa Gracenote katika michezo ya Bundesliga, zinaonyesha kuwa asilimia ya timu kushinda nyumbani kwa hivi sasa imepungua zaidi ya nusu.

Everton wamefanikiwa kupata asilimia 68 ya alama zao 37 wakiwa Goodison msimu huu na Ancelotti hajafungwa katika mechi tano huko.

RTRE